MAZISHI YA MPENDWA WETU MZEE BENJAMINI TINKALIGAILE KIJIJINI IHEMBE-KARAGWE....!
Wanaonekana Watoto wa familia ya mpendwa wetu,Mwalimu wetu Mzee Mzee Benjamini Kabindo Tinkaligaile wakiwa tayari kuweka maua kwenye kaburi la Baba yao mzazi .
Mpendwa wetu Mzee Benjamini Kabindo Tinkaligaile pichani enzi za uhai wake,Marehemu Mwalimu Benjamini Kabindo Tinkaligaile alizaliwa tarehe 13/8/1936 katika kitongoji cha Chibungo Kijiji Ihembe akiwa kifungua mimba wa wazazi wake Sebastiyani Tinkaligaile na Mukabagande ambao kwa sasa nao ni Marehemu
Mchungaji wa Kilutheri akiongoza Ibada ya Mzee wetu Mwalimu Benjamini Kabindo Tinkaligaile
Wazee marafiki wa familia wakishiriki Ibada ya Mpendwa wetu Mwalimu Benjamini Kabindo Tinkaligaile aliyefundisha kwa kipindi cha miaka 35 katika shule za msingi za Lukajange, Murongo, Katembe, Nyabwegila,Nyaruzumbura,Nyakayanja,Ihembe zote za Karagwe,Nyabugera ya Biharamulo,Mubango ya Buganguzi Muleba,Bisheshe,Kibingo,Kahanga ,Lukale na Nyakayanja mpaka kustaafu kwako mwaka 1991.
Taswira umati wa watu ukishiriki Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Mzee Benjamini Kabindo Tinkaligaile
Wanafamilia wakiongoza na Mtoto Mkubwa Bencolias Tinkaligaile pichani katikati
Ndugu wa marehemu mpendwa wetu Mwalimu Benjamini Kabindo Tinkaligaile wakishiriki Ibada hiyo
Muendelezo wa matukio ya picha wakati Ibada ikiendele
Wanafamilia wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya Mpendwa wao Mzee Benjamin Tinkaligaile yaliyofanyika nyumbani kwao Kijijini Ihembe Karagwe
Sehemu ya Waombolezaji waliohudhuria mazishi ya mzee wetu Mwalimu Benjamin Tinkaligaile
Watoto wa mpendwa wtu wakitoa heshima kuaga mwili wa mpendwa Mwalimu Benjamini Kabindo Tinkaligaile
#Tutaonanabadae mpendwa wetu Mzee wetu Benjamini Kabindo Tinkaligaile
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiwa unaendele
Vilio vya machozi vikitawala mahala hapa wakati watoto wa Mpendwa wetu Mzee wetu wanatoa heshima za mwisho
Hakika ni simanzi kubwa kwa wanafamilia wakati wa kutoa heshima zao za mwisho
Kwa heri Baba, kwa heri mwalimu, kwa heri mlezi wetu
Wasifu wa Mzee wetu Benjamini Kabindo Tinkaligaile ukisomwa
Marehemu Mzee Benjamini Kabindo Tinkaligaile katika Uhai wake Mungu alimjalia kuzaa watoto wa kiume tisa na wa kike Sita mpaka umauti unamkuta ameacha watoto hai 12,wakiume 6 na wa kike 6.
Kama desturi kwa mtu yeyote mashuhuri Mwalimu Benjamini Kabindo Tinkaligaile alipewa majina mbalimbali (Ebikubya) kulingana na nyakati na harakati za maisha yake, majina hayo ni Bilanzi,Biikula,Kinanga Mikono,Rutaka,Babu na Roho yangu.
'Mkama we Byembo' mtamboni akiwajibika
Watu ni wengi kweli kweli waliopata kuhudhuria mazishi hayo.
Muendelezo wa matukio ya picha.
Umati mkubwa wa waombolezaji wakishiriki Ibada ya mazishi ya Mzee wetu Benjamini Tinkaligaile.
Kaka Benko akitoa neno la Shukrani kwa watu wote na waliowafariji kwa njia moja ama nyingine
Wanafamilia wakati wa Utambulisho.
Kaka Mkubwa Bencolias akitoa Utambulisho kwa familia yake na familia ya mzee wake aliyejipatia umaarufu kwa kuacha kumbukumbu ya kitabu chenye historia ya Ukoo wa 'Abeilili' wa Wilayani Karagwe
Kaka Bencolias akitoa utambulisho kwa mke wake na Kijana wake
Utambulisho kwa wanafamilia ukiendelea
Muendelezo wa matukio ya picha mazishi ya Mpendwa Mwalimu Benjamini Tinkaligaile
Mjane wa Marehemu Mzee Benjamini Tinkaligaile katikati akiwa na ndugu zake wakati wa utambulisho.
Watoto wa Marehemu wakiongozwa na Kaka yao Bencolias Tinkaligaile wakiweka shada la maua
Mmoja wa Wajukuu akiweka shada la Maua
Mama Mjane wa Marehemu wakati akielekea kuweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa mme wake
Meneja wa Tanroads Mkoa Kagera akiweka shada laa maua kwenye kaburi la mpendwa wetu Mzee Benjamin Tinkaligaile
Meneja wa Tanroads Mkoa Kagera akiweka shada laa maua kwenye kaburi la mpendwa wetu Mzee Benjamin Tinkaligaile
Eneo la kaburi matukio ya picha mazishi ya Mpendwa Mwalimu Benjamini Tinkaligaile
Utaratibu wa kuweka mashada kwenye kaburi la mpendwa wetu ukiendelea.
Watoto wa marehemu kwa pamoja wakiwa tayari kuweka mishumaa kwenye kaburi
Watoto wa marehemu kwa pamoja na wanafamilia wakiwa tayari kuweka mishumaa kwenye kaburi
Eneo la kaburi wakati utaratibu wa kuweka mashada unaendelea
Bwana BekaTinkaligaile pichani kulia akifarijiana na marafiki wa familia.
Salaam za rambirambi zikiendelea.
Benck na Beka Tinkaligaile pichani
Salaam za rambirambi kutoka kwa wana Ihembe waishio Muleba
Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya mwisho ya Maisha ya mpendwa wetu Mzee Benjamini Kabindo Tinkaligaile
Meneja wa Tanroads Mkoa Kagera akitoa salaam za rambirambi
Moja wa mwanafunzi aliyepata kufundishwa na Mwalimu Benjamin Tinkaligaile
Waombolezaji wakiwafariji wafiwa
Katika kuwafariji Wafiwa kufuatia msiba huu mkubwa
#Bukobawadau tunatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huu mkubwa,Daima Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele mzee wetu Benjamin Tinkaligaile
Muendelezo wa matukio ya picha mazishi ya Mpendwa Mwalimu Benjamini Tinkaligaile
Muendelezo wa matukio ya picha mazishi ya Mpendwa Mwalimu Benjamini Tinkaligaile
Akitoa Salaam za rambirambi kwa niaba ya Chama cha mapinduzi na kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Karagwe Mhe.Innocent Bashungwa
Mkono wa pole kutoka kwa Kiongozi wa UVCCM Karagwe kwa niaba ya Chama na kwa niaba Mbunge wa Karagwe Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa.
Muendelezo wa matukio ya picha mazishi ya Mpendwa Mwalimu Benjamini Tinkaligaile
Mwisho #Bukobawadau tunatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huu mkubwa,Daima Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele mzee wetu,Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe amen....!