MAZISHI YA DR EMMANUEL RWAMUSHAIJA NYUMBANI KWAKE KAMACHUMU NDOLAGE
Mamia ya Waombolezaji wameungana na familia ya Marehemu Dkt Emmanuel Titus Rwamushaija katika mazishi ya mpendwa wetu Dkt Emmanuel Rwamushaisha aliyewahi kufanya kazi katika hospitali mbalimbali , mashirika na taasisi za kimataifa
Baadhi ya wanafamilia ya Mpendwa wetu Dkt Emmanuel maarufu katika familia kama (Mjomba) wakiwa katika picha ya pamoja muda mchache kabla ya taratibu za Ibada ya mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake kijijini Ndolage Kamachumu
Watoto wawili wa kuzaliwa na mpendwa wetu Dkt Emmanuel Rwamushaija.
Katika maisha yake Marehemu Dkt Emmanuel alibahatika kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuteuliwa na Wizara ya ya Afya kuomgoza timu ya Madaktari/Wataalam ambayo ilipelekwa msumbiji chini ya mpango wa msaada kwa nchi hiyo kukombolewa kutoka ukoloni wa Wareno
Mapema kabla ya Ibada ya mazishi ,sehemu ya wanafamilia wakiwa katika picha kwa ajili ya kumbukumbu
Mapema kabla ya Ibada ya mazishi ,sehemu ya wanafamilia wakiwa katika picha kwa ajili ya kumbukumbu
Endelea kuwa nasi kwa matukio ya picha kutoka Ndolage -Kamachumu,Mazishi ya Mpendwa wetu Dkt Emmanuel Rwamushaija
Dr George na Mr John Gagoro katika hili na lile
Mwanzo wa Ibada ya mazishi ya moendwa wetu Dkt Emmanuel Titus Rwamushaija
Ms Catheline pole sana kwa kumpoteza Mjomba
Msafara Wakati jeneza likitolewa ndani nyumbani kwa marehemu Dkt Emaanuel Rwamushaja kuelekea ukumbini kwa ajili ya Ibada ya maziko
Msafara kuelekea ukumbini kwa ajili ya Ibada ya mazishi hayo.
Mama Mjane wa marehemu Dr.Emmanuel Rwamushaija
Ndugu Frank Mutayoba akishiriki Ibada ya mazishi hayo
Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Dkt Emanuel ikiendelea
Muendelezo wa matukio ya picha
Mama Muhazi pichani
Watoto wa Mpendwa wetu wakisoma wasifu wa Baba yao;'Kama watoto wa marehemu tutamkumbuka sana Baba Yetu kwa mazuri na msukumu mkubwa aliotupa maishani,Daima alisema na kusisitiza tulenge kufikia kilele cha mafanikio makubwa katika maisha.
"Baba yetu alisisitiza Daima tuwe waaminifu na wanyenyekevu kwa watu,alitufundisha kuwa na upendo kwa watu wote na kuheshimu na kuthamini familia yetu,alikuwa mtetezi mkubwa wa mshikamano wa ndugu na familia Tutamkosa Baba Yetu"
Rafiki wa familia kutoka nchini Uganda akitoa salaam zake za rambirambi
Salaam zarambirambu kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanafamilia na marafiki wa familia .
Mwenyekiti wa kamati ya Mazishi Mzee Masabala pichani akitoa neno l shukrani
Endelea kuwa nasi kwa mtiriko mzima wa matukio ya picha
Neno la shukrani kwa niaba ya familia likitolewa.
Salaam za rambirambi kutoka nchini Rwanda
Katika hili na lile wakati ratiba ikiendelea
Mzee Yusto Mchuruza akitoa salaam zake za rambirambi kama rafiki wa familia
Dr.George pichani
Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu likiingizwa kwenye kaburi
Mjukuu waMarehemu Dkt Emmanuel akiweka Udongo
Mzee Masabala ambaye ni mwenyekiti wa mazishi hayo akiweka shada la maua
Utaratibu wa kuweka mashada ukiendelea
Utaratibu wa kuweka mashada ukiendelea
Familia ya Mzee Balyagati ikiweka Shada la maua
Mtoto wa marehemu mpendwa wetu Dkt Emmanuel Rwamushaija akiwa tayari kuweka mshumua kwenye kaburi
Wanafamilia wakiwa tayari kwa ajili ya kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la mpendwa wao.
Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu mara baada ya mazishi
Muendelezo wa matukio ya picha Mazishi ya Mpendwa wetu Dr.Emmanuel Rwamushaija
Katika maisha yake Marehemu Dkt Emmanuel alibahatika kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuteuliwa na Wizara ya ya Afya kuomgoza timu ya Madaktari/Wataalam ambayo ilipelekwa msumbiji chini ya mpango wa msaada kwa nchi hiyo kukombolewa kutoka ukoloni wa Wareno na badae alifanya kazi katika Hospital na mashirika mbalimbali mpaka mwaka 2005.
Bukobawadau tunatoa pole kwa familia ya Marehemu Dkt Emmanuel Titus Rwamushaija Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.Ameen!!