A FINAL GOODBYE FOR MZEE PAUL BASHEREKA IN PICTURES
Baba yetu mpendwa Mzee Paul Bashereka tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi ndipo tarehe 5/4/2020 tukiwa katika mfungu wa kwarezima amekuita kwenye makazi yake ya milele,baba yetu mpendwa tutaendelea kukuombea siku zote za maisha yetu hapa duniani tutakukumbuka kila siku iitwayo leo kwani pengo uliloliacha halitazibika kamwe hasa kwa upole,ucheshi,ukarimu na busara zako
Baba yetu umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza, imani umeilinda; hatimaye umelala. Bwana akupe pumziko jema!.
Baba yetu Mzee Paul Bashereka umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza, imani umeilinda; hatimaye umelala. Bwana akupe pumziko jema!..Raha ya milele umpe eeh bwana na mwanga wa milele umuangazie,roho yake ipumzike pumzika kwa Amani
Sehemu ya wanafamilia wakishiriki Ibada ya mazishi ya Mpendwa wao Mzee Paul Rweyemamu Bashereka (88)
Baba Askofu Kilaini akitoa neno na kumuombea Mzee Paul Bashereka
Taswira mbalimbali Ibada ya Mazishi mpendwa wetu Mzee Paul Bashereka ikiwa inaendelea nyumbani kwake Kitendaguro Bukoba
Fr. Bandio wa Parokia ya Rwamishenyi akiongoza Ibada ya Mazishi ya Mpendwa wetu Mzee Paul Bashereka.
Katika hali ya Simanzi ananekana Mzee Matungwa na Mama yake Mzazi (Ma Bernaidina )Mama mjane wa Mpendwa mzee Paul Bashereka
Kushoto ni Mama wadogo wa Familia hii,ndugu zake na Ma Bernaidina
Waombolezaji wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya Mzee Paul Bashereka...
Taswira waombolezaja wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya Mpendwa Mzee Paul Bashereka.
Mzee Godwin Rwezaula akitoa neno kwa niaba ya wanaukoo..
Umoja wa wanamama wa Bukoba Town wakiwa tayari kukabidhi rambirambi zao kwa Mama Adventina Matungwa ambaye ni mwanachama mwenzao
Mama Matungwa akipokea rambirambi hizo kutoka kwa Mama Mhazi kwa niaba ya wanachama wenzake
Muendelezo wa matukio ya picha...Mazishi ya Mzee Bashereka,Kitendaguro Bukoba.
Muendelezo wa matukio ya pichayaliyojiri katika Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Mzee Paul Bashereka
Chief Kalumuna akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Umoja wao..
Mzee Lupia akiongea machache kabla ya kutoa Salaam za rambirambi
Picha inazungumza mengi.....tunawaombea subira na Mwenyezi Mungu ailaze roho Mzee wetu mahala pema peponi
Kwa tanakali na Style yenye ya aina yake kutoka kwa Ndugu Novatus Nkwamawakati akitoa salaam za rambirambi .
...Macho na Masikio yakielekezwa kwa Ndugu Novatus Nkwama.....
Ndugu Novatus Nkwamaa kimkabidhi Ubani kwa Mzee Matungwa kaka mkubwa wa familia hii
Romwad Bashereka akitoa shukrani kwa marafiki zake waliomfikishia rambirambi...
Wasifu wa Mpendwa wetu ukisomwa na Dada Matrida...
Bi Jamila akitoa salaam za rambirambi kwa familia
Mzee Robart Matungwa akitoa nen la shukrani kwa niaba ya familia.
Bi Beatrice akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya familia ya Lujwangana.
Al Masoud Kamala Kalumuna akikabidhi rambirambi yake
Baba Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini akiongoza zoezi la kutoa heshima za mwisho kuuaga Mwili wa Mpendwa wetu mzee Paul Bashereka
Padre alieongoza Ibada ya Mazishi haya Fr. Bandio wa Parokia ya Rwamishenyi akitoa heshima za mwisho
Fr. Rwanzo na Fr Lomward Mkandala
Last respect....Mama Bernaidina akiwa ameongozana na Watoto wake...
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea kwa wana familia
Gilbart Bashereka (Last born) akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa baba yake ...
Dada Liberatha na Mdogo wake Matilda machozi yakiwatoka wakati wa kutoa heshima za mwisho mpendwa wao.
Dada Liberatha tunakuombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzkatika simanzi kubwa wakati wa kutoa heshima zake za mwisho...
Dada Tima akiwa karibu sana na Liberatha
Tunawaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.....
Poleni sana ndugu tunawaombea ustahimilivu mkubwa katika kipindi hili kigumu
Dada Parveen Williams wakati wa kutoa heshima za mwisho
Kaka Medard Bashereka akitoa heshima za mwisho .
Wanafamilia wakitoa heshima zao za mwisho kuaga Mwili wa Mpendwa wao Baba yao,Mlezi wao Mzee Paul Bashereka......
Muendelezo wa matukio ya picha wakati wa zoezi la kutoa heshima za mwisho
Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho
Sehemu ya Wajukuu wakitoa heshima za mwisho msiba wa Babu yao mpendwa...
Taswira mbalimbali waombolezaji wakiendelea na utaratibu wa kutoa heshima zao za mwisho
Waltar Matungwa akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa Babu yake Mzee Paul Bashereka.
Kuelekea eneo la kaburi kumpumzisha mzee wetu
Kuelekea eneo la kaburi kumpumzisha mzee wetu
Tayari kwa jeneza kushushwa kaburini
Pata muendelezo wa matukio ya picha eneo la kaburi.....
Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya mwisho ya Maisha ya mpendwa wetu mzee Paul Bashereka
Mama yetu Ma Bernaidina Bashereka akiweka Udongo kwenye kaburi la Mme wake
Wanafamilia wakiweka Udongo kwenye kaburi la Mzee wetu Paul Bashereka..
Padre akiwa tayari kuweka msalaba kwenye kaburi la Mpendwa wetu Baba yetu Mzee Paul Bashereka
Baba paroko Fr Bandio na msaidizi wake Fr Rwazo.
Watoto wa mpendwa wetu Mzee Paul Bashereka wakiweka shada la maua kwa pamoja..
Wakwe wa familia wakiweka Shada la maua kwa pamoja
Wakwe wa familia ya mpendwa wetu Mzee Paul Bashereka mara baada ya kuweka shada la maua.
Bi Benna akiweka Shada la maua.
Adv.Protas Ishengoma akiweka shada la maua...
Mama Mdogo Tima katika utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiwa unaendelea.....
Ndugu Laurean Bwanakunu akiwa tayari kuweka shada la maua..
Akiweka shada la maua pichani ni Bwana Laurean Bwanakun
Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea kwa kuzingatia makundi mbalimbali
Wawakilishi wa familia ya Lujwangana wakiwa tayari kuweka shada la maua
Utaratibu wa kuweka Mashada ya maua unaendelea.... Pichani ni Mzee Godwin Rwezaula
Mama Mgole Shop akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mzee Paul Bashereka
Mh.Chief Kalumuna akiweka shada la maua...
Mzee Lupia,Mrungi Badru na Adv Ishengoma wakiweka shada la maua
Katunzi na Amon kwa niaba ya wajukuu wa familia ya Mzee Bashereka wakiwa tayari kuweka shada la maua.
Dada Naima rafiki wa karibu wa familia akiweka Shada la maua.
Kwa maana twajua kwamba kama hema hii tunamoishi tukiwa ulimwenguni itaharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba ya milele ;Wakorintho 5
Kutoka kushoto pichani ni Febronia Bashereka,Domina Bashereka,Matilda Bashereka na Liberatha Bashereka,watoto wa kike wa mpendwa wetu Mzee Paul Kashereka
Edgar na Sunday majirani wa familia ni baadhi ya waombolezaji walioshiriki mazishi hayo yaliyofanyika Kitendaguro Manispaa Bukoba.
Marafiki wa familia pichani kushoto ni Donasco Kilaja.
Ndugu jamaa na marafiki katika picha ya pamoja na wanafamilia ya Mpendwa wetu Paul Bashereka...
Pichani kulia kabisa ni Mrs Merdad Bashereka ( Mama Amon) akifuatia na Naima na Grace marafiki wa karibu wa familia hii
Dada Naima,Dada Libe na Dada Fortunata wakibadilishana mawazo.
Jane na Lesper George mara baada ya kushiriki mazishi ya Babu yao Mpendwa
Mama Achi Hamis na Dada Matrida Bashereka katika picha ya pamoja...
Kuzungumza na kusaidiana ndio urafiki wa kweli... Pichani anaonekana Dada Naima akimfariji rafiki yake Dada Libe Bashereka
Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu mara baada ya Mazishi ya Mzee wetu Mzee Paul Bashereka
Poleni sana Ndugu ...tunawaombea subira na Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi,Apumzike kwa Amani Mzee Bashereka
Marafiki wa familia katika picha maalumu ya kumbukumbu na Dada Domina Bashereka.
Parveen Williams pichani..
Mwisho Kaka Merdard akizungumza Wazujuu wa familia mbele ya na Camera yetu,Raha ya milele umpe eeh bwana na mwanga wa milele umuangazie,apumzika kwa Amani Mzee Bashereka...