#GERA UZINDUZI WA MAFUNZO MAALUM YA VIJANA YA KUJENGA UWEZO WA KUWEZA KUJIAJIRI
Viongozi
wanaowania nafasi za uongozi wametakiwa kufanya maendeleo ambayo
yataacha alama kwa vizazi vilivyopo na vijavyo na kuepukana na tabia za
kuharibu miradi na miundombinu ya watangulizi wao
Wito
huo umetolewa na Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (MNEC) Kagera Ndugu
Wilbroad pichani.
Mh.Mtabuzi wakati akifungua mafunzo maalum ya vijana zaidi ya 200
yatakayotolewa kwa miezi mitatu katika kozi maalum kwa Vijana ya
kujenga uwezo wa kuweza kujiajiri ;Elimu ya Ujasiriamali, Ujenzi, ufundi
ushonaji ,umeme ,Ufugaji Nyuki ,Kompyuta na kilimo .Mh.Balozi Kamala akiteta jambo na Mh.Msafiri Nyme na Mh. William Osward Lutta
Mafunzo
hayo ambayo yamefadhiliwa na Mbunge Balozi Dr.Deodurus Kamala yanalenga
kuwafikia zaidi ya vijana 1,000 ambao hawakuweza kupata nafasi au Uwezo
wa kuendelea na masomo baada ya kuhitimu Elimu ya msingi na Sekondari.
"Huu
ni uongozi unaoacha alama,kama MTU atajifunzia fani Fulani
atawafundishaa na wengine atawakomboa Ndugu,nachukia MTU anayetaka
uongozi kwa kuharibu miradi ya MTU mwingine ,huyo afai kuwa kiongozi"
amesema Mutabuzi
Mmoja kati ya Wazazi aliyeongozana na Kijana wake katika usahili wa awamu ya kwanza.
Katika picha ya pamoja na wanafunzi waliopokelewa chuoni hapo Jumapili ya leo
Baadhi wa Vijana mara baada ya kuwasili Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Gera
Mnec Wilbroad pichani na Balozi Dr.Kamala mara baada ya kufanikisha utaratibu wa kuwakomboa Vijana Wilayani Missenyi kwa kuanzisha Mafunzo maalum ya kuwajengea uwezi waweze kujiajiri.