PUMZIKA MZEE FRANCIS B. BAYONA (1919-2021)
Sehemu ya wanafamilia wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Mzee Francis Bayona
Marehemu Mzee Francis Bayona alipata elimu ya Msingi kwenye shule ya White Sisters,Mugana darasa la kwanza hadi la tatu kama ilivyokuwa kawaida kwa wakati huo.
Mzee Francis Bayona mwaka 1943-1945 alienda vita kuu ya pili ya Dunia ambapo alipigana hadi nchini Kenya na ABYSSINIA ambayo ndiyo Ethiopoa ya sasa.
Taswira mbalimbali msibani hapo muda mchache kabla ya Ibada ya Mazishi ya Mpendwa wetu Mzee Francis Bayona ambaye alipata kufanya kazi katika kampuni ya David Burrow Dar es Salaam ambapo alikuwa incharge wa wa kitengo cha plumbing,Kampuni iliyokuwa ikifanya kazi za ujenzi na Serikali wakati huo.
Mwaka
1952 alirudi nyumbani na kufungua Duka la biashara jirani na
Nyakijoga.Mwaka 1956-1975 alipata ajira Bukoba Town Council akiwa kama
fundi bomba mkuu hadi alipostaafu mwaka 1975 na kurudi kijijini
kuendelea na shughili za kilimo hadi mwisho wa maisha yake.
Marehemu Mzee Francis amejaliwa wajukuu 52,Vitukuu 78 na Vilembwe 108.
Marehemu Mzee Francis alikuwa mtu wa Ibada na hodari katika Imani ,alikuwa mwanachama wa shirika la Wafransico waliojulikana sana kama Watersial aliojiunga nao tangu mwaka 1950,Aliweza kushiriki Ibada za Misa siku zote hata katika uzee wake.
Tumuombee pumziko la Amani Mzee wetu...!
Padre Deodatus Tiba akitolea jambo ufafanuzi wakati wa Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Mzee Francis Berchmans Bayona.
Baba Askofu Almachius Vincent Rweyongeza wa Jimbo katoliki Kayanga akiongoza zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wetu.Umati wa waombolezaji wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika Kitongoji cha Rugaze,Kijiji Kantare parokia ya Mugana kushiriki mazishi ya Mzee Francis Berchmans Bayona (102)
Padre Karumuna akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya wana Bwanjai waishio mikoani
Watoto wa Marehemu Mzee Francis Bayona wakiwa wameungana na wanafamilia wengine pamoja na waombolezaji katika Ibada ya Mazishi ya Mzee Francis Bayona
Mapadre wakitoa heshima za mwisho kwa Mzee wetu Mzee Francis Bayona ,Mzee aliyekuwa na karama ya uvumilivu na ustahimilivu maisha yake yote.
Padre Deodatus Tiba Paroko wa Parokia ya Mugana akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wetu Mzee Francis Bayona
Muendelezo wa matukio ya picha Marafiki wa marehemu wakitoa heshima zao za mwisho
Mzee Pontian Kashangaki Msemaji wa familia akisoma wasifu wa marehemu Mzee Francis Bayona na kutoa utambulisho kwa wanafamilia...
Mzee Wincheslaus Bayona ambaye ni mtoto wa kwanza wa marehemu Mzee Frances Bayona
Mzee Elizeus Bayona mwenye umri wa miaka 67 mmoja kati wa watoto wa kuzaliwa na Marehemu mzee Francis Bayona
Mtoto wa marehemu pichani wakati utambulishgo ukiwa unaendelea
Watoto wa Marehemu Mzee Francis wakati zoezi la utambulisho linaendelea..
Eng. Lambert Bayona wakati wa utambulisho
Utambulisho ukiendelea kwa watoto wa marehemu Mzee Francis Bayona
Ma Anatoria (82) ambaye ni Dada wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Francis Bayona
Mwongozaji wa shughuli nzima ya mazishi ya Mpendwa wetu.
Sister Joyce Imelda akiweka shada la maua...
Wanafamilia wakiendelea kuweka mashada kwenye kaburi la mpendwa wetu.
Prof Kaijage akiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa Mzee Francis Bayona (1919-2021)
Eng Theodory Bayona na mke wake wakiweka shada la maua
Bi Oliver Bayona akiweka Sawa shada la maua kwenye kaburi la mkwe wake.
Muendelezo wa matukio ya picha wakati utaratibu wa kuweka mashada ukiendelea..
Ndugu Bosco Bayona ambaye ni mjukuu wa marehemu mzee Francis Bayona akiweka shada la maua
Mtoto wa mwisho wa kiume kuzaliwa na Marehemu Mzee Francis Bayona,Eng Lambert Bayona na mke wake wakiweka shada la maua kwenye kaburi.
Baadhi ya wajukuu wakiweka shada la maua..Padre Karumuna kama mwana ukoo akitoa neno..
Mh. Focas akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Bwanjai Community Group
Muendelezo wa matukio ya picha.
Salaam za rambirambi zikitolewa na Padre Anthony Lugundiza
Salaam za rambirambi zikendelea
Wawakilishi wa makundi mbalimbali wakiendelea kutoa salaam za rambirambi kifo cha Mpendwa mzee Francis Bayona
Vilio na machozi vikitawala kwa wanafamilia...
Simanzi ,vilio na machozi vikiendelea kutawala...
Hivi ndivyo hali ilivyokua katika Mazishi ya mpendwa wetu mzee Francis Bayona
Tangulia Mzee wetu ,Vita umeipigana na mwendo umeumaliza.
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiwa unaendelea...
Wakwe wa familia hii kwa pamoja wakitoa heshima zao za mwisho
Mzee Paschal B. Kabukoba ambaye ni mdogo wa marehemu Mzee Francis Bayona akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili ya mpendwa kaka yake.
Katikati ni mdogo wake Marehemu Mzee Francis B.Bayona,
Eng Lambert Bayona akitoa heshima zake za mwisho
Eng Theodory Bayona wakati wa kutoa heshima za mwisho
Prof Kilama rafiki wa familia katika last respect kwa mpendwa wetu
Muendelezo wa matukio ya picha
Picha wakati wa kutoa heshima za mwisho
Umati wa waombolezaji katika mstari kumuaga mpendwa wetu Mzee Francis Bayona (102)
Lily,Brenda na Anna baadhi ya wajukuu wa Marehemu Mzee Francis Bayona wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Babu yao
Padre Tiba Baba paroko ya porokia ya mugana...
Taswira mara baada ya mazishi ya mzee wetu Mzee Francis Bayona
Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu.
Baadhi ya wajukuu katika picha ya kumbukumbu mara baada ya mazishi ya mpendwa mzee Francis Bayona
Wazee wakibadilishana mawazo mara baada ya mazishi ya mpendwa wetu Mzee Francis Bayona.Familia inatumia furasa hii kutoa shukrani za dhati kwa masista wa Kanosa (hawapo pichani) kwa huduma yao nzuri na madaktari waliojitahidi kuokoa maisha ya mzee wetu hususani wa hospitali ya Mugana
Katika hali ya simanzi anaonekana mdogo wa Marehemu Mzee Francis Bayona pichani kulia.
Kushoto pichani ni Mzee Wincheslaus Bayona, mtoto mkubwa wa marehemu Mzee Francis Bayona, kwa sasa mzee huyu ana umri wa miaka 78.
Watawa wa kikatoliki wa Parokia ya Mugana ambao ni marafiki wa M pendwa wetu Mzee Francis Bayona wakiwa katika picha ya pamoja na Mrs Oliver Bayona mara baada ya kumpumzisha mpendwa Mzee Francis Bayona.
Sehemu ya waombolezaji pichani kulia ni Mzee Yusuph Ngaiza
Muendelezo wa matukio ya picha Mazishi ya Mzee Francis Bayona