DKT. YONAZI ASEMA NENDENI MKATEKELEZE KWA VITENDO MAFUNZO MLIYOPEWA
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi
akizungumza kwa njia ya mkutano mtandao (video conference) na wataalam kutoka
Halmashauri mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar wakati akifunga mafunzo ya
kuwajengea uwezo wataalamu hao ya
utekelezaji wa anwani za makazi katika mkutano uliofanyika leo ofisi za TTCL,
jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi
akizungumza kwa njia ya mkutano mtandao (video conference) na wataalam kutoka
Halmashauri mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar wakati akifunga mafunzo ya
kuwajengea uwezo wataalamu hao ya
utekelezaji wa anwani za makazi katika mkutano uliofanyika leo ofisi za TTCL,
jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dorosela Rugaiyamu akizungumza kwa njia ya mkutano mtandao (video conference) na wataalam wa Halmashauri mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar wakati Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi kulia) akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu kwa ajili ya kutekeleza anwani za makazi katika mkutano uliofanyika leo ofisi za TTCL, jijini Dodoma. \
Viongozi na
wataalam waliopo kwenye vituo vinne vya mikoa ya Mwanza, Mbeya, Tanga na
Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya anwani
za makazi na postikodi kwa wataalam hao kwa njia ya mkutano mtandao wakati
akiwa ofisi za TTCL, jijini Dodoma
DKT. YONAZI ASEMA
NENDENI MKATEKELEZE KWA VITENDO MAFUNZO MLIYOPEWA
à
Wataalam
422 wa Tanzania Bara, Zanzibar Wapatiwa Mafunzo ya Anwani za Makazi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Dkt. Jim Yonazi amefunga mafunzo ya utekelezaji wa anwani za makazi na
postikodi kwa njia ya mkutano mtandao kwa wataalam wa Tanzania Bara na Zanzibar
yaliyofanyika kwenye vituo vinne vya mkoa wa Mwanza, Mbeya, Tanga na Zanzibar
Dkt. Yonazi amewataka wataalam hao 422 waliopatiwa mafunzo hayo ambapo wataalam 389 wametoka Tanzania Bara na 33 wametoka Zanzibar kwenda kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo kwa kuweka namba za nyumba, majina ya mitaa na barabara kwenye halmashauri wanazotoka ili kuhakikisha kuwa anwani za makazi zinatekelezwa nchi nzima na kukamilika ifikapo mwezi Mei mwaka huu
Ameongeza kuwa utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi utasaidia
kufungua kasi ya uchumi, utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi na kuifungua
Tanzania kidijitali, “mwananchi yeyote atatambulika duniani na anaweza kufikiwa
na mteja kwa ajili ya kuuza bidhaa au huduma, hivyo kila mwananchi awiwe kuwa
na namba ya nyumba, jina la barabara au mtaa anapoishi,” amesema Dkt. Yonazi
Pia, ametoa wito kwa kampuni, wadau mbali mbali na familia kuchangia
utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi na kila mmoja awe balozi wa anwani
za makazi na wataalam watoe taarifa kwa viongozi wao na Wizara iko tayari
kuendelea kushirikiana kutekeleza hili
Naye Mratibu wa Kitaifa wa Anwani za Makazi na Postikodi wa Wizara hiyo, Mhandisi Jampyion Mbugi, amesema kuwa wataalam waliopatiwa mafunzo hayo ni wataalam wawili kutoka kwenye kila halmashauri nchi nzima ambapo inahusisha wataalam wa TEHAMA, Ardhi, Mipango Miji na Ramani ambapo wamepatiwa mafunzo hayo kwa muda wa wiki moja
kuanzia tarehe 17 Januari mwaka huu ya utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi ikiwemo kuweka namba za nyumba, jina la mtaa au barabara na kuweka taarifa za maeneo hayo kwenye mfumo wa kielektroniki wa NAPA ili anwani hizo zipatikane na kutumiwa na wananchi kwa kuwawezesha kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya wataalam wengine waliopatiwa mafunzo hayo, Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Kilindi, Tanga ndugu Anastius Biswalo Manumbu amesema kuwa wamepatiwa mafunzo hayo kwa vitendo na wataenda kuwafundisha wataalam wengine ili kuhakikisha kuwa anwani za makazi zinakamilika kwa wakati kuendana na azma ya Serikali na watazingatia miongozo iliyopo ya uwekaji wa anwani za makazi na postikodi
Ufungaji huo wa mafunzo ya anwani za makazi na postikodi nchini, umehudhuriwa
na viongozi mbali mbali wa vituo vinne ambapo mafunzo hayo yametolewa ikiwemo wawakilishi
wa wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa mikoa ya Tanga, Mwanza, Mbeya na Zazibar
ambapo kwa upande wa Zanzibar waliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ndugu Amour
Bakari
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini,
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari