Bukobawadau

#MULEBA BANK YA TCB YAIPIGA JEKI SERIKALI SEKTA YA ELIMU YAKABIDHI VYUMBA VIWILI VYA MADARASA, MADAWATI 50 NA CHOO

Muleba-Kagera.

Bank ya Biashara Tanzania TCB imetenga Milioni 500 kwa mwaka 2022 kwa ajili ya kuboresha Miundombinu ya Elimu ,Afya na ustawi wa jamii Kama sehemu ya kuishukuru jamii kwa kuchagua Bank hiyo.

Meneja wa huduma kwa wafanya Biashara wakubwa kutoka bank ya TCB Adrophina William  amesema bank hiyo imekuwa ya muda mrefu ambapo ilianza Kama bank ya posta na Sasa na Bank ya Biashara  inatambua mchango mkubwa na mwitikio mkubwa kwa jamii inayojitokeza kupata huduma mbalimbali katika bank hiyo hivyo faida inayopatikana inapaswa kurudi kuinufaisha jamii.

Bi Adolphina William  pichani Meneja wa huduma kwa wafanya Biashara wakubwa wa Bank ya TCB
Majingo ya Vyumba viwili vya madara ya Shule ya Msingi Kitunga Wilayani Muleba liyokabidhiwa na Bank ya TCB.
Uongozi wa Bank hiyo umekabidhi  vyumba viwili vya madarasa vya kisasa katika shule ya msingi  Kitunga Wilayani  Muleba ,Vyoo vya walimu na madawati 50 vyenye thamani ya shilingi Milioni 36.2  Kama sehemu ya kurudisha Fadhila kwa jamii na kuwataka wanafunzi wa shule hiyo kutunza Miundombinu na kuongeza chachu  ya ufahulu katika masomo yao.
Katibu Tawala Mkoa Kagera tawala wa mkoa Kagera Profesa Faistine Kamuzora licha ya kutoa shukurani zake kwa bank hiyo ya TCB ameitaka Bank hiyo kutoa Elimu sahihi ya mikopo kwa walimu ambao wamekuwa wakijiingiza katika mikopo umiza na baadhi kushindwa kujikimu inapofika mwisho wa mwezi.

Profesa Kamuzora amesma;Shule hiyo iliyofadhiliwa inaingia katika  idadi yenye shule zenye majengo yenye ubora na yanayovutia  huku akisema kuwa shule hiyo itaondokana na uhaba wa madawati ambapo amehaidi kutoa vitabu katika shule hiyo Kama sehemu ya mchango wake .

Samson Kayange Meneja wa Bank ya TCB Tawi la Bukoba akitolea akiongea na wanahabari
Grolia Mutta na Erick Swai wafanyakazi wa Bank ya TCB
Ukaguzi wa Madawati 50 yaliyokabidhiwa Shule ya Msingi Kitunga Wilayani Muleba
Tanzania Commercial Bank Kama Benki ya Biashara ya Tanzania yumeamua kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuinua na kukuza kiwango cha elimu nchini
Vyumba vya Madara
Jengo la Choo kilichokabidhiwa na Tanzania Commercial Bank kwa Shule ya Msingi Kitunga Wilaya Muleba
Taswira eneo la tukio hafla ya makabidhiano Shule ya Msingi Kitunga Wilaya Muleba
Taswira mbalimbali kupitia picha na Bukobawadau
Katibu tawala wa Mkoa Kagera Prof.Kamuzora akiongozana na Maofisa wa Bank ya TCB Kukagua Vyumba vya Madarasa .
Muendelzo wa matukio ya picha
Burudani ya Ngoma kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitunga iliyopo Wilaya ya Muleba.
Mwenywekiti wa Kijiji Bushole Dominic Damician wakati akisoma lisala kwa Mgeni Rasmi.
Leonard Mafuru Mfanyakazi wa Tanzania Commercial Bank akiwajibika kama Mc muongozaji wa hafla ya makabidhiano .
Mwalimu Hashimu Kibaizi Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kitunga Wilaya Muleba
Taswira mbalimbali kupitia picha na Bukobawadau
Zawadi ya Mbuzi aliyekabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji Tanzania Commercial Bank 
Erick Swai na Amani Nassari Meneja wa Uendeshaji Bank ya TCB Tawi la Bukoba
Picha mbalimbali kwa ajili ya Kumbukumbu
Maofisa wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB katikapicha ya pamoja naUongozi wa Serikali,Katibu tawala wa Mkoa Kagera Prof.Kamuzora.
Next Post Previous Post
Bukobawadau