JENGO LA MAMA NA MTOTO KUKABIDHIWA MWEZI MACHI MWAKA HUU
Muonekano wa nje ya jengo jipya
la Mama na Mtoto katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa - Sekou Toure linalojengwa na
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao ujenzi wake umefikia asilimia 94. Jengo
hilo linagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 10.1 na kutarajiwa kuanza kutumia
mwezi Machi, 2022.
Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, akizungumza na Kaimu Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachuzibwa, wakati akitoka kukagua
ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika hospital ya Rufaa ya Mkoa - Sekou Toure
linalotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, akitoa maelekezo kwa Kaimu
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoa wa Mwanza Eng. Moses Urio,
alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospital ya Rufaa ya
Mkoa - Sekou Toure linalotekelezwa na
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mkoani Mwanza.
Kaimu Meneja wa Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA), mkoa wa Mwanza Eng. Moses Urio, akifafanua jambo kwa Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, wakati
alipokagua maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika
Hospital ya Rufaa ya Mkoa - Sekou Toure
linalotekelezwa na Wakala huo, mkoani humo.
PICHA
NA WUU