ZIARA YA BALOZI WA SWEDEN NCHINI TANZANIA NA UONGOZI WA REPOA WILAYA YA MULEBA - KAGERA
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg akipata ufafanuzi kutoka kwa Dr.Jane wa Repoa kuhusu zawadi ya Shuka iliyotolewa kwake na kikundi cha wakinamama na Maendeleo Wilayani Muleba ambao ni wanufaika wa miradi inayodhaminiwa na Sweden.Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg na Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Dkt. Donald Mmari wakiongea na Mkutugenzi wa Muhola Bwn.Saulo Marauli.
Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmari (pichani kushoto) akitoa taarifa ya utafiti wa hali ya umaskini kwa Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg katika kikao kilichofanyika kwnye Jengo la Mkuu wa Wilaya Muleba Mkoani Kagera.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bw.anders Sjorberg akipokea zawadi kutoka kwa Katibu mwenezi wa CCM Kata -Magata Wilaya ya Muleba Bw Mansoor Amri,Balozi wa Sweden nchi ni Tanzania Bw.Anders Sjorberg ametembelea Miradi mbalimbali na kukutana na Wanufaika wa Mdadi wa TASAF Wilaya Muleba unaoratibiwa na SERIKALI.
Muendelezo wa matukio ya picha ziara ya Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg Wilayani Muleba.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg katika picha ya pamoja na baadhi wa Wanamama wa Kijiji cha Katanga Kata ya Magata wilayani Muleba, Kagera ambao ni wanufaika wa mradi wa TASAF.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bw.anders Sjorberg akipokea zawadi kutoka kwa Katibu mwenezi wa CCM Kata -Magata Wilaya ya Muleba Bw Mansoor Amri,Balozi wa Sweden nchi ni Tanzania Bw.Anders Sjorberg ametembelea Miradi mbalimbali na kukutana na Wanufaika wa Mdadi wa TASAF Wilaya Muleba unaoratibiwa na SERIKALI.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bw.anders Sjorberg akipokea zawadi kutoka kwa Katibu mwenezi wa CCM Kata -Magata Wilaya ya Muleba Bw Mansoor Amri,Balozi wa Sweden nchi ni Tanzania Bw.Anders Sjorberg ametembelea Miradi mbalimbali na kukutana na Wanufaika wa Mdadi wa TASAF Wilaya Muleba unaoratibiwa na SERIKALI.
Baadhi ya Wanamama Wanufaika wa TASAF wa Kijiji cha Katanga Wilaya ya Muleba.
Kikundi Cha Akina mama na maendeleo Wilayani Muleba kinachojihusisha na uchakataji wa mazao ya uvuvi kimeomba ufadhili wa kupata mitambo ya kukausha Dagaa na samaki nyakati za mvua ili kurahisisha shughuli zao za uchakataji.
Balozi wa Swedeni Nchini Tanzania Anders Sjobergy ametembelea vikundi vya wanawake wanahojihusha na shughuli mbalimbali kupitia ufadhili wa Swedeni na kuona namna wanawake wanavyojiingizia kipato kutokana na kazi zao.
Mwenyekiti wa kikundi icho Jovitha Justiniani amemwambia Balozi huyo kuwa licha ya Changamoto ya mvua ambayo imekuwa ikikwamisha ufanisi wa kazi yao lakini bado hawajakata tamaa bado wanaendelea kupambana na umasikini ingawa Kama wangepata mtambo wa kukausha mazao ya ziwani wangepiga hatua kubwa.
Shughuli zilizokaguliwa na Balozi huyo na kupata maelezo ya kina Ni Uongezaji thamani wa mazao ya ziwani ,vikundi vya stadi za mkomo Kama Ufumaji na uchongaji unaofanywa na wanawake ambapo Balozi huyo amewatia Moyo kuondokana na umasikini Ni Hali ya udhubutu wa kufanya kila unachokiamini.
Shughuli za wanawake ambao hujiingiazia kipato kupitia vikundi mbalimbali mkoani Kagera zimekuwa zikisimamiwa na REPOA Taasisi inayohusika na utafiti wa kaya masikini pamoja na mafunzo yanaholenga kukomboa kaya hizo kutoka hatua moja Hadi nyingine.
Balozi huyo ametembelea Wilaya ya Muleba na Karagwe na kukagua shughuli mbalimbali ambazo zinafadhiliwa na ubalozi wa Swedeni Nchini Tanzania.