CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI TRC NA TAZARA KUPATIWA UFUMBUZI
CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI TRC NA TAZARA KUPATIWA UFUMBUZI
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Atupele
Mwakibete, amesema Sekta ya Uchukuzi iko katika hatua mbalimbali za
kushughulikia changamoto za watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na
Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuongeza tija kwa taasisi
hizo.
Naibu Waziri Mwakibete ametoa kauli hiyo
alipotembelea karakana ya kutengeneza vichwa na mabehewa ya TRC Mkoani
Morogoro na kusisitiza Serikali itaendelea kuwekeza kwenye taasisi hizo ili
kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji nchini.

“Changamoto za kitumishi ambazo zimekuwa zikiendelea
hapa nataka niwahakikishie kuwa zitatatuliwa na mtapata mrejesho kupitia
viongozi wa taasisi, ninaamini zikishughulikiwa kwa kiasi kikubwa zitachangia
mabadiliko kiutendaji” amesema Naibu Waziri Mwakibete.
Naibu waziri Mwakibete ametumia nafasi hiyo
kuwapongeza wafanyakazi wa karakana hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi na
kujituma wakiwa na lengo la kuhakikisha kazi hazisimami katika karakana hiyo.
Aidha, Naibu Waziri Mwakibete amewasisitiza watumishi
hao kufanya ukarabati wa vichwa na mabehewa kwa kuzingatia thamani ya fedha ili
uwekezaji unaofanywa ufanyike kwa makini ili kufanya viendelee kutoa huduma za
uhakika na salama.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Albert Magandi, amesema mpaka sasa kupitia
watumishi hao wameweza kukarabati vichwa vya treni takribani kumi na
Sita kwa ajili kusafirisha mizigo na abiria na vichwa saba kwa
ajili ya treni za sogeza.
Naye Mmoja wa watumishi wa karakana hiyo, Bw.
Vedastus Lugega, amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa pamoja na changamoto
mbalimbali zilizopo Wafanyakazi wako tayari kuendelea kuhakikisha
ukarabati unafanywa kwa wakati na kuzingatia viwango ili kutohujumu Serikali.
Naibu Waziri Mwakibete yuko Mkoani Morogoro kwa ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya miradi ya sekta ya uchukuzi ikiwemo mradi wa ukarabati wa vichwa na mabehewa.
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)