UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIGOMA KUANZA KUJENGWA
Mhandisi Mshauri wa Kampuni
ya Norplan, anayesimamia ujenzi wa barabara ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1)
kwa kiwango cha lami, Eng. Henry Ngogolo, akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi
na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya wakati alipokuwa akikagua
mradi huo, mkoani Kigoma
UJENZI
WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIGOMA KUANZA KUJENGWA
Serikali imekwishaanza
usanifu wa barabara ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha
Kigoma kutoka mita 1,800 uliopo hivi sasa hadi kufikia mita 3,000 ili kuwezesha
ndege kubwa kama vile Bombadier Q400 na Boeing kutua bila changamoto yoyote.
Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, amezungumza hayo mkoani
Kigoma akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
kimkakati inayoendelea.
“Tunategemea uboreshaji wa
Kiwanja cha Ndege cha Kigoma uanze mwaka huu wa fedha 2021/22 ambapo hadi sasa
tupo katika hatua ya manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi”, amesema Naibu
Waziri huyo.
ndege, jengo la zimamoto,
barabara za kuingia na kutoka uwanja wa ndege na taa za kuongozea ndege wakati
wa usiku.
Ameongeza kuwa lengo kuu la Serikali
ni kufanya Kiwanja hicho kifanye kazi masaa 24.
“Lengo kubwa la Serikali ni
kuifungua mkoa wa Kigoma kwa njia ya anga, barabara, reli na maji”, amesisitiza
Eng. Kasekenya.
Katika hatua nyingine, Naibu
Waziri Kasekenya amekagua ujenzi wa barabara ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1), kwa
kiwango cha lami na kusisitiza kwa Wakandarasi kuongeza vifaa, wafanyakazi
pamoja na kupanga mpango kazi mpya wa kutekeleza miradi hiyo usiku na mchana.
“Barabara hizi tuzikamilisha
tutakuwa tumemaliza changamoto ya vumbi kuanzia Kigoma, Uvinza, Urambo, Tabora
hadi Manyoni na kuelekea hadi Mji wa Serikali wa Dodoma”, amefafanua Eng.
Kasekenya.
Naye Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma, ameeleza kuwa ujenzi wa
barabara ya Uvinza - Malagarasi kwa kiwango cha lami unagharimu shilingi
Bilioni 62 na utekelezaji wake ni miezi 24.
Ukamilikaji wa miradi hiyo
ya kimkakati katika Mkoa wa Kigoma ni moja ya azma ya Serikali katika kufungua
mkoa huo ambao ndio lango kuu la biashara kati ya Tanzania na nchi za DRC,
Burundi na Rwanda.