ZAIDI YA BILIONI 460 KUFUNGUA MKOA WA KIGOMA KWA BARABARA ZA LAMI
PICHA
NA WUU
ZAIDI
YA BILIONI 460 KUFUNGUA MKOA WA KIGOMA KWA BARABARA ZA LAMI
Serikali imepanga kutumia zaidi
ya shilingi Bilioni 460 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa miundombinu ya
barabara kwa kiwango cha lami ili kuweza kuufungua kibiashara na kuchochea fursa
nyingi za kimaendeleo katika mkoa wa Kigoma.
Aidha, Bilioni 21 zimetolewa
kwa ajili ya miradi mingine ya nyongeza ambayo itagusa jamii inayozunguka
katika miradi ikiwemo ujenzi wa wa Shule, Soko, Miundombinu ya Maji Safi na Taka
na Vituo cha Mabasi katika wilaya za Buhigwe, Kasulu na Kibondo.
Naibu Waziri huyo amezitaja
barabara ambazo zinatekelezwa kwa fedha hizo ikiwa ni ujenzi wa barabara ya
Njia panda ya Nduta – Kabingo (km 62.5), Njiapanda ya Nduta – Kibondo Mjini (km
25.9), Mvugwe – Njiapanda ya Nduta (km 59.35), Kanyani – Kidyama – Mvugwe (km
70.5), Njia panda ya Kasulu – Manyovu (km 68.25) ambazo zinatarajiwa kukamilika
ifikapo mwezi Oktoba, 2023.
“Serikali imeamua kuweka
wakandarasi wengi katika mkoa huu kwa kuwa Kigoma haukuwa umefunguka kwa
barabara za lami sasa zimeanza kujengwa hivyo tunawajibu kama wananchi kulinda
miundombinu hii na kujiweka tayari kwa kufanya biashara na mikoa mingine ya
jirani ili kujiongezea kipato”, amefafanua Kasekenya.
Katika kufungua mkoa wa
Kigoma na Katavi, Eng. Kasekenya amesema kuwa tayari mkandarasi amekwishaanza
ujenzi kutokea Mpanda (km 50) kuelekea Uvinza ili kupunguza umbali wa safari
ukitokea Katavi.
“Tuna barabara tatu kubwa ambazo zinaunganisha
mkoa wa Kigoma na mikoa mingine ambazo ni barabara ya Kibondo, Tabora, na
Mpanda na tayari wakandarasi wamekwishanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha
lami”, ameeleza Naibu Waziri Kasekenya
Naye Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma, amemuahidi Naibu Waziri
huyo kuwasimamia wakandarasi wote waliopo katika maeneo mbalimbali mkoani humo
ili kuhakikisha mkoa wa Kigoma unafunguka na kurahasisha shughuli za
usafirishaji na mikoa jirani pamoja na nchi jirani.
“Nikuhakikishie Naibu Waziri
TANROADS tuko bega kwa bega kusimamia miradi hii licha ya changamoto za mvua na
zinginezo watakamilisha kwa wakati na ubora uliosanifiwa”, amesema Eng. Choma.
Naibu Waziri Kasekenya yupo
mkoani Kigoma katika ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya utelezaji wa
miradi ya kimkakati inayoendelea mkoani humo.