Bukobawadau

UMATI WAMZIKA MA ROZALIA KAMALA MAMA MZAZI WA BALOZI DKT KAMALA

Jana tumempumzisha Mpendwa wetu Ma Rozalia Nyangoma Kamala kwenye nyumba yake ya milele nyumbani kwa familia Kijijini Bwanjai-Mugana . Mungu amlaze mahali pema peponi.
Mapadre wakiongoza Ibada ya Mazishi ya Mpendwa wetu Mama yetu,Mlezi na rafiki Ma Rozalia Kamala yaliyofanyika Jana Jumamosi Aug 20,2022 Nyumbani kwa familia kijijini Bwanjai-Mugana Wilayani Missenyi na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji.
Wanafamilia wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya mpendwa wao Ma Rozalia Nyangoma Kamala.
Umati wa waombolezaji wakiwa wameungana na wanafamilia katika Ibada ya Misa takatifu ya Mazishi ya Ma Rozalia Kamala
 
Waombolezi wakiwa katika Misa ya Mazishi ya Mpendwa Ma Rozalia Kamala aliyetutoka baada kusumbuliwa na maradhi kwa muda mfupi na ametibiwa katika hospitali mbali mbali zikiwemo Gaumeht Bukoba, Bugando Mwanza na baadae kuhamishiwa Ocean Road Dar es Salaam hadi umauti ulipomkuta tarehe 16/8/2022.
Familia inatoa  shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki mazishi haya na Mapadre wote waliompa huduma za kiroho, hospitali zote alizotibiwa, ndugu, jamaa na marafiki.


Hakika ni simanzi kubwa kwa ndugu wa familia ya Ma Rozalia Kamala
Muendelezo wa matukio ya picha wakati zoezi la kutoa heshima za mwisho likiendelea
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea...
Muongozaji wa Maziko haya ndugu Optaty Henry akihakikisha kila jambo linaenda vyema kwa mjibu wa ratiba...
Utaratibu wa kutoa hshima za mwisho ukiendelea kwa watu wote.
Muda mchache kabla ya kuelekea eneo la Makaburi ...
Msafara ukielekea eneo la makaburi..

Inaendelea.....

Safari ya Mwisho ya Maisha ya Mpendwa Ma Rozalia Kamala.
Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu Ma Rozalia Nyangoma Kamala likiingizwa kaburini..
Mzee Bilikwiza akishiriki mazishi ya Dada yake mpndwa Ma Rozalia Kamala
Wanafamilia ya Ishengoma wakiwa wamempoteza Shangazi yao mpendwa.

Wajukuu wa mpendwa wetu Ma Rozalia Kamala katika nyuso za huzuni.

Watoto wa kuzaliwa na Mpendwa Ma Rozalia Nyangoma Kamala wakiwa tayari kuweka shada la maua




Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Projestus Tegamaisho akitoa mkono wa pole kwa Balozi Dkt Kamala
Katika hili na lile anaonekana Dr Frenk Ludigo akibadilishana mawazo na waombolezaji waliofika kuwafariji.
Dr Frenk Ludigo akibadilishana mawazo na waombolezaji waliofika kuwafariji.

Muendelezo wa matukio ya picha mara baada ya mazishi
Mulangila Divo Rugaibula pichani
Bwana Charles rafiki wa familia.
Taswira mbalimbali kutoka kijijini Bwanjai-Mugana Mazishi ya Ma Rozalia Kamala
Muendelezo wa matukio ya picha,Mazishi ya Ma Rozalia Kamala.
Mwijage's wakiwa wameshiriki msiba wa Shangazi yao Mpendwa Ma Rozalia Kamala
Balozi Dkt Kamala akibadilishana mawazo na Prof.Kamuzora aliyefika kuwafariji wafiwa kufuatia msiba wa Mama yao mzazi
Marafika wa Dada Lita Kamala katika picha ya kumbukumbu
Mama Amida Sued na Bi Lita Kamala pichani
Mwalimu Ivonna na Mama Banyenza wakitoa mkono wa pole kwa wafiwa
Mwalimu Ivonna na Mama Banyenza wakitoa mkono wa pole na Ubani kwa Balozi dkt Kamala.
Marafiki wa familia Mwalimu Ivonna na Mama Banyenza wakitoa mkono wa pole kwa wafiwa.

WASIFU WA MAREHEMU MAMA YETU ROZALIA KAMALA 

Marehemu mama yetu Ma Rozalia Kamala alizaliwa mnamo tarehe 17/10/1940 katika familia ya Mzee Joseph Bikoche Bilikwija na Ma Madgalena Mukaite katika kitongoji cha Katunga kijijini Kikukwe kata ya Kanyigi.

Alibatizwa mnamo tarehe 19/10/1940 katika parokia ya Bugombe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kanyigo na ambapo alikomunika na kupata kipaimara.

ELIMU

Alisoma elimu ya msingi na alihitimu darasa la nane mnamo mwaka 1956 katika shule ya msingi Bugombe. Baada ya elimu ya msingi alijiunga na chuo cha uuguzi/ ukunga 1/10/1960 Musoma mkoani Mara na alihitimu mnamo mwaka 1963.

AJIRA

Aliajiriwa kama muuguzi/ mkunga daraja la III mwaka 1963 na alistaafu mnamo mwaka 1995 akiwa muuguzi daraja la I. 

NDOA

Marehemu mama yetu alifunga ndoa takatifu na Marehemu baba yetu Pastory Stanslaus Kamala  mnamo mwaka 1965 katika kanisa katoliki St. John Bosco Bukoba. Mama alibaatika kupata Watoto 3 ambao ni Ritha Kamala, Diodorus Kamala na Redempta Kamala.

UUMINI

Mama yetu amekuwa mama wa sala kila wakati na alikuwa Katibu wa Chama wa Kitume cha Bikira Maria wa Mateso Saba kiparokia, kidekamia hadi ngazi ya jumuiya. 

ITIKADI

Mama alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi, UWT ngazi ya wilaya, mjumbe kamati ya siasa ya kata, mjumbe wa siasa ya Tawi Rwamashonga kadi yake ikiwa No. Aa-220748.

KUUGUA

Mama amesumbuliwa na maradhi kwa muda mfupi na ametibiwa katika hospitali mbali mbali zikiwemo Gaumeht Bukoba, Bugando Mwanza na baadae kuhamishiwa Ocean Road Dar es Salaam hadi umauti ulipomkuta tarehe 16/8/2022.

Tunatoa shukrani kwa Mapadre wote waliompa huduma za kiroho, hospitali zote alizotibiwa, ndugu, jamaa na marafiki.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe milele!

Next Post Previous Post
Bukobawadau