SERIKALI YAWATOA HOFU WAFANYABISHARA
Sehemu ya Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Sekta Binafsi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao cha Wadau cha Maboresho ya Bandari ya Tanga (Tanga Port Improvement Committee), Mhandisi Aron Kisaka (hayupo pichani), wakati wa kikao cha wadau hao kilichofanyika hivi karibuni jijini Tanga
Mkurugenzi
wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi
Aron Kisaka (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga,
Mhandisi Masoud Mrisha (mwenye Kaunda suti nyeusi), wakati alipokagua maendeleo
ya ukarabati wa reli inayoingia Bandari ya Tanga jijini humo hivi karibuni.
Kichwa
cha treni chenye namba 8801-TRL kikifanya majaribio kwenye njia ya relu kuingia
katika Bandari ya Tanga.
Picha na WUU
SERIKALI YAWATOA HOFU WAFANYABISHARA
Serikali
imewahakikishia wafanyabiashara wa mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na
Manyara kuwa itaendelea kuboresha miundombinu na mifumo ya usafirishaji ili
kurahisisha shughuli za usafiri na usarishaji wa abiria na mizigo baina ya
mikoa hiyo na nchi jirani.
Akizungumza jjini Tanga mara baada ya ukaguzi wa maboresho ya reli inayoingia bandari ya Tanga Mkurugenzi wa Huduma za Huduma za Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho ya Bandari ya Tanga, Mhandisi Aron Kisaka, amesema kukamilika kwa ukarabati na kukabidhiwa kwa sehemu ya gati lenye mita 300 lazima uende sambamba na maboresho ya miundombinu mingine ili kurahisisha utoaji wa mizigo bandarini.
“Kama
wataalam tunazingatia sana utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yote hatuwezi
kuboresha bandari hii tukaacha kutizama miundombinu saidizi iko kwenye hali
gani, kwa hatua hii iliyofikiwa matokeo yameanza kuonekana ambapo ongezeko la
mizigo kwa mwezi Septemba kwenda Oktoba limefika asilimia 41%,” alisisitiza
Mha. Kisaka
Mhandisi
Kisaka amesema lengo la Bandari ni kuhakikisha mzigo unaingia na kutoka kwa
haraka ili kuongeza ufanisi na kuongeza zaidi shehena ya mzigo unaohudumiwa na
bandari hiyo.
unasimamiwa
kwa karibu na unatarajiwa kukamilika mwezi aprili mwakani.
Mha.
Mrisha ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi pamoja na miundombinu mingine bandarini
hapo kutawezesha zaidi ya tani zaidi ya milioni mbili kwa mwaka na
kutasababisha kushuka kwa bei za bidhaa mbalimbali sokoni.
Naye
Mhandisi Patience Karumuna (wa kwanza kulia) kutoka Shirika la Reli Nchini (TRC)
amesema kazi ya ukarabati wa reli kutoka stesheni ya Tanga mpaka bandarini
ilikuwa umeshakamilka na kichwa cha treni kufanya majaribio lengo likiwa
kubaini mapungufu yaliyobaki baada ya ukarabati.
(Imetolewa
na kitengo cha habari na mawasiliano Serikalini Wizara ya ujenzi na uchukuzi)