Bukobawadau

POSTA BUKOBA YAIMARISHA USALAMA MAHALI PA KAZI

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Bukoba, wakufunzi kutoka Jeshi la zima moto na msimamizi Ndugu Akida Njama wa Kitengo cha Usalama na Upelezi Makao Makuu ya Shirika la Posta na Meneja wa Mkoa Kagera Ndugu Joseph Mutatina baada ya mafunzo ya kuzima moto.

Katika kuimarisha usalama mahali pa kazi Shirika la Posta Tanzania Ofisi ya Bukoba leo tarehe 1/3/2023 wameendesha mafunzo ya kuzima moto.
Mafunzo hayo yamendeshwa na Sgt Shabani Musa (Afisa Habari Mkoa wa Kagera, Kikosi cha Zima Moto) na FC Mwikwabe Mwikwabe (Afisa Zimamoto) yakisimamiwa na Mr. Akida Njama wa kutoka kitengo cha Usalama na upelelezi Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania na Mr. Joseph Mutatina, Meneja wa Mkoa wa Kagera Shirika la Posta Tanzania.


Mafunzo haya yamefanyika mahususi kwa ajili ya malengo makuu yafuatayo:
1. Kuimarisha huduma bora na usalama wa mizigo ya wateja na wao wawapo ndani ya Ofisi za Posta. Hii ni kuwahakikishia wateja kuwa barua, vifurushi na fedha zao wanazotuma kupitia Ofisi za Posta ziko salama hata likitokea janga la moto
2. Kuwajengea uwezo watumishi wa Shirika la Posta Tanzania Mkoa wa Kagera jinsi ya kutumia vizima moto vilivyosimikwa kwenye ofisi za Posta.
3. Kuwahakikishia wapangaji wetu usalama wao na mali zao.
4. Kutekeleza Sheria ya usalama mahala pa kazi.

Wafanyakazi wote wa Posta Bukoba pamoja na walinzi walipata mafunzo hayo Darasani na baadae kwa vitendo. Katika kupata mafunzo hayo kwa vitendo wafanyakazi kwa kuelekezwa na mkufunzi Sgt Shabani walizima moto huo.
Katika zoezi la kwanza la kuzima moto ulizimwa na Ndugu Mbaraka Ibrahim, Msimamizi wa ofisi ya uchambuzi wa barua. Katika zoezi la pili moto ulizimwa na Ridester Paschal ambaye ni Afisa Masoko na zoezi la tatu ulizimwa na Angelica Salvatory ambaye ni mlinzi wa Shirika la Posta Bukoba. Waliozima moto walionyesha umahiri mkubwa kwenye kuzima moto hivyo kuonyesha kufunzu mafunzo yaliyotolewa leo.

Meneja wa Posta Mkoa wa Kagera Ndugu Joseph Mutatina alielezea huduma za Posta kuwa ni usafirishaji wa barua na vifurushi kwa njia ya kawaida, usafirishaji wa barua na vifurushi kwa njia ya haraka (EMS), kusafirisha sampuli za maabara, usafirishaji wa vipeto, Posta mlangoni na mizigo mikubwa (Postcargo), Duka mtandao ambapo hadi sasa tuna maduka mtandao yapatayo 800 nchi nzima, huduma za internet, kupangisha majumba na viwanja, uwakala wa fedha na Benki, uwakala wa Bima na uuzaji wa tiketi za ndege za ATCL.
Meneja wa Mkoa ametoa wito kwa wateja wetu kuendelea kutumia huduma za Posta kwani zinatolewa kwa weledi mkubwa, kwa usalama wa hali ya juu na tunauzoefu wa miaka mingi. Amesisitiza wafanyabishara kujiandiandikisha kwenye huduma yetu mpya ya duka mtandao kwani ni bure na biashara zao zitaweza kuonekana duniani kote.

Picha ya wafanyakazi wa Posta wakisiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya nadharia

Mafunzi wakiendelea,Picha ya wanaonekana wafanyakazi wa Posta wakisiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya nadharia.
Sgt Shabani Musa (Afisa Habari Mkoa wa Kagera, Kikosi cha Zima Moto)akiendelea kutoa mafunzo.

Mafunzo yakiendelea

Miss Ridester Paschal akizima moto wakati wa mafunzo kwa vitendo.

Ndg Mbaraka akizima moto wakati wa mafunzo kwa vitendo.

Miss Angelica Salvatory akizima moto wakati wa mafunzo wa vitendo.

Miss Angelica Salvatory akizima moto wakati wa mafunzo wa vitendo.

Katika picha ya pamoja Wafanyakazi wa Shirika la Posta Bukoba, wakufunzi kutoka Jeshi la zima moto na msimamizi Ndugu Akida Njama wa Kitengo cha Usalama na Upelezi Makao Makuu ya Shirika la Posta na Meneja wa Mkoa Kagera Ndugu Joseph Mutatina baada ya mafunzo ya kuzima moto.
 

 
 
 
 
 

Next Post Previous Post
Bukobawadau