NAIBU WAZIRI WA FEDHA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA UINGEREZA.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe.
Hamad Hassan Chande, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Worldline kutoka Ufaransa, Bi. Caroline Jesequel, inayojihusisha na
masuala ya utengenezaji wa mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao, ambae
yupo nchini nchini na ujumbe wake kujifunza na kuona mazingira wezeshi
ya uwekezaji kwa njia ya mtandao katika Sekta ya Benki na kwenye Taasisi
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi Ndogo ya Hazina, jijini Dar
es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, na ujumbe wake, wakifuatilia wasilisho wakati wa mkutano wake na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Worldline kutoka Ufaransa Bi. Caroline Jesequel, inayojihusisha na masuala ya utengenezaji wa mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao Ofisi Ndogo ya Hazina, jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bw. Japhet Justine, na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Huduma za Tehama, Dkt. John Sausi.
Naibu Waziri wa Fedha,
Mhe. Hamad Hassan Chande, akiteta jambo na Kamishna wa Idara ya
Usimamizi wa Deni la Serikali Bw. Japhet Justine wakati wa kikao na
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wordline kutoka Ufaransa Bi. Caroline
Jesequel (hayupo pichani), Ofisi Ndogo ya Hazina, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali WFM - DSM)
Na. Josephine Majura, WF, Dar es Salaam
Serikali
imewaalika wadau wa Sekta Binafsi kutoka Uingereza kuwekeza nchini ili
kusaidia juhudi za Serikali kufikia malengo yake.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande,
alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa
Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey.
Mhe.
Chande alisema Serikali imekamilisha utiaji saini na UK Export Finance
kwenye Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na kuendeleza
barabara ya Tunguu - Makunduchi -kilomita 28, Fumba - Kisauni-Mazizini
-kilomita 13.2, na mkoani - Chake Chake and Pemba Airport kwa ukubwa wa
kilomita 43.5
.
Katika
kikao hicho Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Chande aliwakaribisha Wawekezaji
mbalimbali kutoka Uingereza kuja kuwekeza katika sekta za uzalishaji,
uongezaji thamani na utalii nchini Tanzania.
“Nakukaribisha wewe na wafanyabiashara na wawekezaji wa kiingereza kuleta mitaji yenu Tanzania ” alisema Chande.
Kwa
upande wake Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya
Uingereza Mhe. John Humphrey Humphrey, alisema watashirikiana na
Serikali kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika
na kuendekeza kuwekeza katika vipaumbele vya kibiashara vilivyopo
nchini Tanzania.
MWISHO