POSTA KAGERA WAFANYA KIKAO KAZI KUKUMBUSHANA MALENGO 2023/24
Mwenyekiti wa kikao ambaye ndiye Meneja wa Mkoa ndugu Joseph Mutatina alieleza madhumuni ya kikao kuwa ni kama ifuatavyo:
1. Kupata uelewa wa pamoja wa wafanyakazi wa Posta juu ya malengo na mipango ya Shirika Kwa mwaka wa fedha 2023/24
2.Kupata taarifa ya utendaji kazi Kwa mwaka wa fedha 2022/23
3. Kujadili na kuelewa pamoja upimo wa utendaji kazi Kwa Kila mfanyakazi
4. Kuweka mikakati ya kuongeza mapato ya pamoja na Kila wilaya moja moja.
5. Kuwa na uelewa wa pamoja juu ya Mpango Mkakati wa 8 wa Shirika wa Mwaka 2022- 2026 ambao unasisitiza ukuaji wa Biashara Kwa kutumia Posta ya kidigitali.
Kikao kilianza Kwa sala ya Shirika iliyofuatiwa na mada ya Afya ya
akili iliyotolewa na mtoa mada ndugu Issa Mrimi kutoka ofisi ya Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Ndugu Issa Mrimi alisisitiza kuepuka msongo wa
mawazo.alieleza kuwa ukiwa na msongo wa mawazo huwezi kutimiza majukumu
yako ipasavyo yakiwa Niya kifamilia na kiofisi vilevile. Alieleza jinsi
ya kuepuka msongo wa mawazo na jinsi kumsaidia mtu mwenye msongo Kwa
kutoa msaada wa awali na inaposhindikana kumpa rufaa.
Katika
kikao kazi hicho Meneja wa Mkoa Ndugu Joseph Mutatina, alisisitiza Kila
mtumishi wa Posta kuwa na uelewa wa huduma zote za Posta.Pia
alisisitiza Kila mtumishi kuwa balozi mzuri wa Posta ili kuinua kismati
Cha Shirika.
Huduma za Shirika la Posta ni pamoja na
kusafirisha barua na vifurushi Kwa njia ya haraka, kusafirisha barua na
vifurushi Kwa Kwa njia ya kawaida, huduma za Uwakala wa mabenki,
mitandao ya simu, bima na kuuza tiketi za ndege, huduma ya kusafirisha
sampuli za binadamu, huduma za internet, Duka mtandao na huduma za
kukodisha majengo.
Meneja wa Mkoa alisisitiza
watumishi kutumia huduma za kidigitali zinazotolewa na Shirika la Posta.
Aliwaekeza watumishi kuwa Posta inapatikana kwenye mitandao ya Twitter,
Instagram, Facebook na linked. Meneja alisisitiza kuwa mfumo wetu wa
Posta Kiganjani unazidi kuboreshwa na kumpa urahisi mtumiaji.
Meneja wa Mkoa Ndugu Joseph Mutatina (wa pili Toka kulia waliokaa) na kushoto kwake ni msimamizi huduma za Ndugu Antidius Rukwatage.kulia kwake (mwenye Tshirt ya blue) ni mtoa ndugu Issa Mrimi kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na anayefata ni Mhasibu wa Mkoa Ndugu Patrick Mwakasege. Waliosimama ni Postamasta wa ofisi za Posta zilizopo wilayani. Kutoka kulia ni Postamasta wa Kyaka, Ngara, Kamachumu, biharamulo na Muleba
Pichani wanaonekana wajumbe wakati wanasikilizasalamu za Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo Kwa watumishi wote zilizorushwa Moja Kwa Moja kidigitali na kusikilizwa kwenye TV inayonasa mawimbi ya computer bila kutumia waya(wireless)
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Kagera wakati Kikao kazi kiiendelea
Katika Picha ya pamoja baada ya wajumbe kusikiliza salamu za Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo Kwa watumishi wote zilizorushwa Moja Kwa Moja kidigitali na kusikilizwa kwenye TV inayonasa mawimbi ya computer bila kutumia waya(wireless).
Picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano wa Bukoba Coop hoteWafanyakazi wote wa Shirika la Posta Mkoa wa Kagera katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano wa Bukoba Coop hotel mara baada ya kikao Kazi kilichofanyika tarehe 8/8/2023.