RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa
katka Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo jijini Dodoma Machi 25, 2025
katika iftar iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naibu Waziri Mwanaidi alimwakilisha Rais Samia katika shughuli hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akishiriki iftar iliyofanyika kwenye Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo jijini Dodoma Machi 25, 2025 katika iftar iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis i alimwakilisha Rais Samia katika shughuli hiyo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati wa iftar iliyofanyika kwenye Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo jijini Dodoma Machi 25, 2025 katika iftar iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naibu Waziri Mwanaidi alimwakilisha Rais Samia katika shughuli hiyo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akipokea msaada wa vifaa mbalimbali kwaajili ya watoto wanaolelewa kwenye Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo wakati wa iftar iliyofanyika kwenye Makao hayo jijini Dodoma Machi 25, 2025 katika iftar iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naibu Waziri Mwanaidi alimwakilisha Rais Samia katika shughuli hiyo.Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akishiriki iftar iliyofanyika kwenye Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo jijini Dodoma Machi 25, 2025 katika iftar iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis i alimwakilisha Rais Samia katika shughuli hiyo.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
Na WMJJWM- Dodoma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
amewafuturisha Watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Watoto
Kikombo Dodoma katika Kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Akizungumza
wakati wa Iftari hiyo iliyofanyka Machi 25,2025 kwa niaba yake, Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis alitoa shukurani kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka
mazingira wezeshi yenye lengo la kuondoa kabisa changamoto
zinazowakabili watoto walio katika mazingira hatarishi.
“Kipekee
kabisa, ninamshukuru tena Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuweza kufuturisha watoto wanaoishi katika Makao ya Taifa ya Watoto
Kikombo pamoja na maeneo mengine ya nchi hususani Watoto wa Mkoa wa
Arusha na Dar Es Salaam”. ameeleza Naibu Waziri Mwanaidi.
Aidha
aliongeza kuwa Wizara inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na
wadau kwa lengo la kuhakikisha watoto walio katika mazingira hatarishi
wanapatiwa huduma ya malezi ya muda mfupi katika Makao ya Watoto.
“Serikali
na Wadau tutaendelea kushirikiana kutoa huduma kulingana na sheria,
kanuni na miongozo tuliyojiwekea, nitumie fursa hii kuwaomba wamiliki wa
makao ya kulelea watoto kuhakikisha mnatoa huduma kwa mtoto kwa
kuzingatia maslahi mapana ya mtoto”. amesema Naibu Waziri Mwanaidi.
Mhe.
Mwanaidi alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi, walezi na watendaji
wa Wizara kwa kuendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa afua za
malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika makao yote hapa
nchini.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalum Dkt.John Jingu amewasihi watoto waishio katika makao hayo kuishi
kwa upendo na amani huku wakiweka bidii katika masomo yao na stadi za
kazi kwa ujumla ili waweze kufikia malengo yao ya baadae.
Naye
Mwakilishi kutoka Shirika la Abbot fund Edna Hauli ameipongeza Serikali
kwa juhudi zake katika kuhakiksha watoto wanakuwa salama na kuahidi
kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha
watoto wanapata mahitaji yao muhimu na kuweza kufikia utimilifu wao kama
binadamu.
Sanjari na
hilo katika tukio hilo pia kuliambatana na tukio la kukabidhi mashine ya
kufulia 4, printer na photocopy mashine 1, vitabu 1670 friji 2 nguo na
mahitaji mengine ambavyo vilitolewa na Shirika la Abbot Fund vikiwa na
thamani ya shiling Milioni 88 ili viweze kurahisisha majukumu ya
utendaji kazi ndani ya Makao hayo.
MWISHO