”Rasmi Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba lavunjwa”

Soko Kuu la Manispaa Bukoba limevunjwa ili kupisha ujenzi wa soko jipya la kimataifa unaotarajiwa kuanza muda wowote.

Kwa Wakati tofauti wameonekana Wafanyabiashara eneo la SOKO KUU Mjini Bukoba Wakibomoa Mabanda yao ya biashara kupisha Ujenzi wa Soko jipya leo April 12,2025.


